Wauguzi watatiza huduma katika hospitali kuu ya Kenyatta

Emmanuel Terer
By Emmanuel Terer October 15, 2018 07:38 (EAT)
Add as a Preferred Source on Google
Wauguzi watatiza huduma katika hospitali kuu ya Kenyatta
Vocalize Pre-Player Loader

Audio By Vocalize

Shughuli za kawaida katika hospitali kuu ya Kenyatta zilitatizika kwa saa kadhaa hii leo baada ya wauguzi kugoma wakidai kuhofia usalama wao.

Hii ni baada ya mmoja wao kupigwa vibaya na kujeruhiwa na jamaa za mgonjwa aliyeaga dunia alipokuwa akihudumiwa hospitalini.

Wauguzi hao walisusia kazi na kutatiza shughuli muhimu hospitalini wakilalamikia kuvamiwa na kupigwa kwa mmoja wao, Mildred Akinyi ambaye anadaiwa kupigwa siku ya jumamosi katika hospitali hiyo kwa tuhuma za kukosa kumhudumia vyema mgonjwa mmoja aliyekuwa akipokea huduma hospitalini.

Jamaa za mgonjwa huyo walikasirika, mpendwa wao alipofariki.

Mildred ambaye amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Kenyatta ni mmoja kati ya wengine ambao wanasemekana kupigwa na washiriki wa familia za wagonjwa wanaoaga dunia hospitalini.

Washukiwa waliohusika na kitendo cha hivi punde wametiwa mbaroni.

Join the Discussion

Share your perspective with the Citizen Digital community.

Moderation applies

Sign In to Publish

No comments yet

This discussion is waiting for your voice. Be the first to share your thoughts!