Mama ateketea Baringo
Audio By Vocalize
Mwanamke mmoja amefariki kutokana na moto unaoaminika kusababishwa na mlipuko wa jiko la stovu uliosambaa na kuchoma nyumba kadhaa usiku wa kuamkia leo eneo la Bondeni, Baringo ya Kati.
Walioshuhudia wanasema mlipuko huo ulisikika mwendo wa saa sita usiku na kufuatiwa na moto mkubwa uliowashinda kuudhibiti.
Wakaazi wametoa wito kwa idara ya kushughulikia majanga ya moto kaunti ya baringo iwe macho kunapotokea ajali za moto.
Mtu mmoja aliyepata majeraha amepelekwa katika hospitali ya rufaa ya kabarnet kwa matibabu zaidi.

Join the Discussion
Share your perspective with the Citizen Digital community.
No comments yet
This discussion is waiting for your voice. Be the first to share your thoughts!