Watu 4 wakamatwa kwa utapeli Kimilili

Watu wanne wamekamatwa mjini Kimilili kaunti ya Bungoma kwa kupakia upya unga iliyotolewa na serikali kwa bei ya chini kama njia mojawapo ya kukabiliana na ukosefu wa unga uliokuwa ukishuhudiwa humu nchini pamoja na kupunguza gharama ya unga kwa wakenya wote.