Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wahukumiwa miaka 20 gerezani

Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wahukumiwa miaka 20 gerezani

Mahakama ya Mombasa imemhukumu Ahmed Said Ahmed kifungo cha miaka 20 gerezani na faini ya shilingi milioni 8 baada ya kupatikana na hatia ya ulanguzi wa mihadarati aina ya heroin yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 28.

Mahakama hiyo pia imemhukumu mlanguzi Clement Sege ambaye ni raia wa Ushelisheli kifungo cha miaka 10 gerezani sawia na faini ya shilingi milioni 5 baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa aina ya Heroin ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6.

Wawili hao walipatikana na hatia ya ulanguzi wa mihadarati hiyo iliyokuwa imefichwa ndani ya mashua kwa jina Baby Iris kati ya tarehe 9 na 20, Aprili, 2015 katika ufuo wa Kilifi boat Yard kaunti ya Kilifi.

Mashua hiyo ni miongoni mwa vyombo viwili vilivyoharibiwa kwa kulipuliwa baharini kufuatia agizo la rais Uhuru Kenyatta katika vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati nchini.