Kaunti ya Trans Nzoia yalaumiwa kwa mapendeleo

Kufuatia ubaguzi wa ajira katika bunge la kaunti ya Trans Nzoia ambapo wawakilishi wa wadi wameajiri asilimia kubwa ya wafanyikazi kutoka jamii zao katika bunge hilo, mashirika ya kijamii katika kaunti hiyo wanawata wawakilishi hao kujiuzulu kwa kukiuka kifungu cha sita cha katiba kuhusu maadili. Kama anavyoarifu mwanahabari wetu Collins Shitiabayi tume ya maadili na kupambana na ufisadi humu nchini tayari imelimevalia njuga swala hilo.