Rais akamilisha ziara yake eneo la kati

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamehitimisha ziara yao ya siku mbili katika kaunti nne za eneo la kati, ambapo walitangaza kutolewa sh. 2.5b za kuwasaidia wakulima wa kahawa kulipa madeni ambayo mashirika yao yanadaiwa na benki.
Na kando na kuzindua ujenzi wa barabara mbili kuu na kukagua mradi wa kuweka mitambo ya kisasa katika hospitali za kerugoya na murang’a, siasa zilishamiri, huku mikwaruzano ya watakaopeperusha bendera ya jubilee katika nyadhifa mbali mbali mwaka ujao ikijitokeza bayana.