Muswada wa mabadiliko ya IEBC wavuka hatua muhimu

Sasa wawaniaji wa nyadhifa mbali mbali wataobwagwa katika chaguzi za mchujo, hawataweza kuhamia vyama vingine au kuwania kama wawaniaji huru, baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha mswada wa marekebisho ya sheria. Wabunge waliokuwa wakipinga kipengee cha kuharamisha mtindo wa wanasiasa kuhamahama vyama walishindwa kupata idadi ya wabunge kuunga mkono azma yao, huku wabunge wengi wakihiari kufuata maagizo ya vinara wa miungano ya jubilee na cord, walioshinikiza mswada huo upitishwe bila mabadiliko yoyote. Sasa mswada huo, pamoja na ule ya makosa ya uchaguzi, itawasilishwa kwa rais, ili aitie sahihi, na kuwa sheria.