Joho, Omar, Mwaboza, Awiti na shahbal kumenyana

Wanasiasa watano kufikia sasa wameeleza nia yao ya kuwania kitia cha ugavana katika kaunti ya Mombasa mwaka ujao. Ingawa Gavana Joho anaonekana makini kuhifadhi nafasi yake, itambidi kumenyana na wengine wanne akiwemo Seneta Hassan Omar, hasimu wake wa kisiasa Suleiman Shahbal, mbunge wa zamani wa kisauni Anania Mwaboza na mbunge wa sasa wa nyali Hezron Awiti.