Hazina ya NSSF yadaiwa kuporwa Ksh. 72M

Donda la ufisadi linaonekana kuendelea kuvuja zaidi huku tume ya maadili na kupambana na ufisadi sasa ikichunguza sakata ya shilingi milioni sabini na mbili zinazowahusisha maafisa wakuu katika hazina ya kustaafu.

Haya yanajiri huku msako wa kuwatafuta aden harakhe ambaye alikuwa naibu mkurugenzi mkuu wa nys na Hassan Noor aliyesimamia kamati ya zabuni katika wizara ya ugatuzi ukiendelea.