Gavana Wahome Gakuru azikwa kijijini Kirichu kaunti ya Nyeri

Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nyeri Dkt. Patrick Wahome Gakuru amezikwa nyumbani kwake, katika kijiji cha kirichu, eneo bunge la Nyeri Mjini, na kuombolezwa kama kiongozi stadi, mwenye maono, aliyeelewa bayana manufaa ya ugatuzi na stadi wa masuala ya uchumi. Familia yake pia ilipata nafasi ya kumuaga mwana, mume, baba na ndugu, katika hafla ambapo siasa za kitaifa zilipenyeza.