Watu 4 akiwemo mwanamke mmoja wakamatwa kwa tuhuma za wizi
Published on: December 18, 2017 07:57 (EAT)
Audio By Vocalize
Watu wanne akiwemo mwanamke mmoja wanazuiliwa na maafisi polisi kwa tuhuma za wizi katika maeneo ya Kilimani na Kileleshwa. Watu hao ambao walipatikana na funguo mia moja na vifaa vya kuvunja milango wanashukiwa kutekeleza wizi katika maeneo mbalimbali ambapo wakati wa mchana ambapo wenye nyumba hawapo . Maafisa wa polisi wanawataka wananchi kuweka mikakati za kiusalama wanaposafiri kusherekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya.


Leave a Comment