Raila amtaka Rais Kenyatta kujiuzulu
Audio By Vocalize
Muungano wa Nasa unasisitiza hauridhiki na tarehe ya mchuano mpya wa urais, hadi masuala tata kuhusu maandalizi ya mchuano huo yashughulikiwe kikamilifu. Ingawa Nasa imempa kongole mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kwa kuuelekeza mjeledi wake kwa afisa mkuu mtendaji Ezra Chiloba kuhusiana na usimamizi wa uchaguzi wa mwezi ujao, ambao matokeo yake yalibatilishwa na mahakama ya juu, inasisitiza wadau wote wahusishwe katika maandalizi ya uchaguzi mpya wa urais. Lakini kwa upande wake, Jubilee inataka IEBC kuchapa kazi bila kuingiliwa au kushinikizwa na yeyote.


Leave a Comment