Daktari anataka ukeketaji uruhusiwe
Published on: January 17, 2018 08:26 (EAT)
Audio By Vocalize
Je, mwanamke aliyekomaa anaweza kupatiwa fursa ya kujiamulia iwapo angetaka kufanyiwa ukeketaji au la? Na je, sheria inayoharamisha ukeketaji inastahili kubatilishwa? Ndio masuali yanayomkabili Jaji David Kemei anaposikiza kesi inayotaka sheria hiyo kubatilishwa. Daktari Tatu Kamau ambaye amewasilisha kesi hiyo anataka wanawake ambao ni watu wazima kupewa nafasi ya kujiamulia wanachotaka kufanya na mwili wao.


Leave a Comment