Mrithi wa Issack Hassan
Published on: November 19, 2016 08:21 (EAT)
Audio By Vocalize
Mgawanyiko kuhusu iwapo watu watano wanaotizamiwa kuhojiwa ili kuchukua nafasi yake Issack Hassan kama mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini umeanza kuibuka huku baadhi ya wanasiasa wakitaka nafasi hiyo itangazwe upya. Hatua hiyo inakisiwa kuchangiwa na mchakato wa kutaka tarehe ya uchaguzi wa mwaka ujao isogezwe mbele hata hivyo chama cha wanasheria nchini kinapinga kauli hiyo na kusema kuwa sababu zinazotolewa na wanasiasa hazina msingi.


Leave a Comment