Uhuru akosoa sababu za mahakama ya juu kufuta ushindi wake
Published on: September 21, 2017 09:05 (EAT)
Audio By Vocalize
Rais Uhuru Kenyatta ameutaja uamuzi wa mahakama ya juu wa kubatilisha uchaguzi wa urais wa Agosti nane kama mapinduzi ya serikali. Kauli hiyo ameitoa tena baada ya mahakama ya juu inayoongozwa na jaji mkuu David Maraga kusoma uamuzi kamili na kutoa sababu za kubatilisha uchaguzi wa urais. Kulingana na rais, mahakama ya juu haikuchunguza ushahidi uliotolewa na tume ya IEBC.


Leave a Comment