Rais Kenyatta akataa mwito wa mazungumzo na Raila
Published on: December 09, 2017 08:33 (EAT)
Audio By Vocalize
Rais Uhuru Kenyatta amepuuzilia mbali shinikizo la kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kinara wa NASA Raila Odinga, kutafuta suluhu ya suitafahamu ya kisiasa inayolighubika taifa kwa sasa. Kenyatta anasema baada ya chaguzi mbili za urais na kuapishwa kwake kuhudumu kwa muhula wa pili, daftari la nipe nikupe za kisiasa limefungwa, na la sasa ni kufanikisha maendeleo ya kitaifa. Huku kauli yake ikipigwa jeki na naibu wake William Ruto, mabalozi wa kigeni, viongozi wa kidini na wale wa biashara wanasisitiza tiba ni mazungumzo tu.


Leave a Comment