Raila ataka kujua chanzo cha pesa za Jubilee
Audio By Vocalize
Huku jubilee ikikamilisha maandalizi ya uzinduzi wa chama chake kipya, chama cha ODM nacho kimetoa ratiba ya matukio ya hafla ya Jumamosi itakayoandaliwa jijini Mombasa hatua inayooneka kama njia ya kudhibiti makali ya Jubilee. Lakini wazingumza katika kaunti ya Kakamega kwenye siku ya tatau ya ziara ya ODM, viongozi wa chama hicho wamewataka viongozi wa chama kipya cha Jubilee kuwaelezea wakenya walikotoa fedha wanazotumia kuandaa hafla ya siku tatu ya uzinduzi wa chama hicho. Viongozi hao wanadai kwamba chama hicho ni kichanga mno na haiwezekani kiwe na mabilioni ya pesa zinazotumiwa kununua majumba, magari na kugharamia ziara ya wajumbe wanaohudhuria mikutano ya hafla hiyo ya uzinduzi.


Leave a Comment