Mabweni mawili yateketea katika shule ya upili ya Kakamega

Mabweni mawili yateketea katika shule ya upili ya Kakamega

Mabweni mawili ya shule ya kitaifa ya wavulana ya Kakamega yameteketea mapema alfajiri ya leo huku malazi na vifaa vya wanafunzi vikichomeka.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Gerald Orina, mkasa huo ulizuka mwendo wa saa 5.45 asubuhi wakati wanafunzi walikuwa wakihudhuria masomo ya ziada almaarufu kama 'morning preps'.

"Wanafunzi wote wako salama, moto ulizuka wakiwa darasa na kuharibu mali zao ikiwemo magodoro,sare za shule kati ya vitu vingine," akasema Orina.

Daniel Mutsya ambaye ni naibu kamanda Kakamega ya kati na alisema kuwa walipata habari ya moto huo kutoka kwa mwalimu mkuu kabla ya kuandamana na wazima moto hadi shuleni humo ili kuudhibiti.

"Bweni mbili zimechomeka mali ya wanafunzi ikiwemo, kwa sasa hatuwezi tathmini gharama ya hasara ila tumeanzisha uchunguzi kubaini kiini hasa cha moto huo," akasema Mutsya.

Katika siku za hivi majuzi visa vya shule kumechomeka vimekuwa vikigonga vichwa vya habari tetesi zikisema huenda moto hizo zinawashwa na wanafunzi kutokana na wao kuchoshwa na ratiba nzito ya masomo.

Tags:

Mabweni mawili yateketea Kakamega

Want to send us a story? Submit on Wananchi Reporting on the Citizen Digital App or Send an email to wananchi@royalmedia.co.ke or Send an SMS to 25170 or WhatsApp on 0743570000

Leave a Comment

Comments

No comments yet.

latest stories