Sheria kali za uvuvi zawaskuma wavuvi Busia kuasi uvuvi na kuzamia ukulima

Sheria kali za uvuvi zawaskuma wavuvi Busia kuasi uvuvi na kuzamia ukulima

  • Kando na kuhangaishwa na askari, ajali za mara kwa mara majini pamoja na uvamivi wa wanyama wa maji kama vile mamba na kiboko kumechangia wengi wa wavuvi kuiasi shughuli hiyo.
  • Wavuvi hawa pia wamesema kuwa kuingizwa kwa samaki wa China nchini kumeangusha bei ya samaki.
  • Wito wao wametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuingilia kati.

Huenda shughuli za uvuvi katika kisiwa cha port Victoria kaunti ya Busia zikasitishwa kutokana na sheria kali zilizowekwa kudhibiti uvuvi kisiwani humo.

Kisiwa hicho kinafahamika kwa uvuvi wa samaki aina ya tilapia, mbuta na omena na kinapakana na mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania.

Uganda inaongoza kwa wingi wa samaki pamoja na ukubwa wake. Kuwekwa kwa sheria kali kudhibiti shughuli za uvuvi kisiwani humo kunawaangaisha wavuvi, wengi wakionekana kutafuta kazi mbadala kama vile kilimo kujiendeleza kimaisha.

Kulingana na David Ouma, 38 mkaazi eneo bunge la Budalangi ambaye kwa sasa ni mkulima wa mboga baada ya kuiasi ile ya uvuvi anailaumu serikali kwa kuwatenga kila wanaposhikwa na maaskari wa nchi jirani ya Uganda.

“Uganda kuna samaki wengi. Ukivuka mpaka utashikwa nakuteswa na maaskari wa Uganda ambao hukuitisha pesa kabla ya kukuachilia,”akasema Ouma.

Aidha anasema mara wanaposhikwa, jaribio zao za kujaribu kupata usaidizi kutoka kwa idara husika nchini zimekuwa zikigonga mwamba.

“Unaposhikwa, askari wa Uganda hukupeleka mahali kunakoitwa Sigulu hapo utazuiliwa huku familia yako ikiangaika, huku wengine wakipelekwa Bugiri kufungwa,” anasema.

Wanaoshikwa huitishwa hadi shilingi milioni moja za Uganda kabla ya kuachiliwa huku wanaodinda kutoa pesa hizo wakifugwa.

Utumizi wa neti ndogo nchini uganda kumepigwa marufuku. Anaypatkana akiwavuwa samaki wadogo hukamatwa.

“Ni hatia kwa mvuvi kuvua samaki wa chini ya kilo moja nchini Uganda,” akaongezea Ouma.

Aidha, utumizi wa taa wanapovua samaki haswa omena nyakati za usiku kumerahisisha wao kukamatwa kutokana na maaskari hao kutumia mwangaza huo kubaini waliko.

Aburu Buluma, ni mkulima wa mahindi na maharagwe kaunti ya Busia na anailaumu serikali ya kenya kutowajibikia masaibu yao licha ya wao kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu madhila wanazopitia kama wavuvi.

“tulilalamika tukaletewa maaskari waitwao 'coast guard', wao sasa ndio wamekuwa kizingiti kikukuu kwa shughuli hii ya uvuvi, utashikwa mara kwa mara kwa kisingizio ya kukosa 'life jacket', leseni na vitu zingine ambazo ukiangalia utafadhalisha kuacha kazi ya uvuvi,” anasema Buluma.

Kando na kuhangaishwa na askari, ajali za mara kwa mara majini pamoja na uvamivi wa wanyama wa maji kama vile mamba na kiboko kumechangia wengi wa wavuvi kuiasi shughuli hiyo.

Wavuvi hawa pia wamesema kuwa kuingizwa kwa samaki wa China nchini kumeangusha bei ya samaki.

Wito wao wametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuingilia kati.