Watu 18 wafariki kwenye ajali eneo la Moinoni, Baringo

Watu 18 wamethibitishwa kufariki kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika barabara ya Marigat kuelekea Loruk kaunti ya Baringo. Waathiriwa walikuwa wakisafirisha bidhaa zao kutoka eneo la marigat kuelekea kapedo wakitumia lori ya maafisa wa polisi wa utawala.