Wakenya, Wadau mbali mbali watoa maoni kuhusu sheria ya uchaguzi

Kwa siku ya pili, kamati maalum ya bunge imeendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau na wananchi kwa jumla, kuhusu mapendekezo ya kuzifanyia mabadiliko sheria za uchaguzi. Muungano wa sekta ya kibinafsi umependekeza maafikiano baina ya wanasiasa, ili kufanikisha uchaguzi huru na haki, ili kuzikwamua biashara ambazo zimedorora kutokana na tumbojoto la kisiasa. Tume ya IEBC inatarajiwa kufika mbele ya kamati hiyo hapo kesho.