Seneta wa Tharaka Nithi achaguliwa kuwa Naibu Spika Seneti

Senata wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki leo hii ameapishwa kuwa naibu wa spika katika bunge la senati.
Hii ni baada ya masenata sitini na saba kupiga kura na Kithure kunyakua kura thelathini na nane. Kindiki alikuwa anachuana na seneta wa Narok Ledama Olekina kutoka chama cha ODM ambaye alipata kura kumi na saba. Uchaguzi huo ulifanywa mara mbili. Wakati bunge la seneti lilifanya vikao vya kwanza wiki iliyopita, aliyekuwa gavana wa Bungoma, Ken Lusaka alichaguliwa kuwa Spika baada ya kumshinda Farah Maalim wa Wiper kwa wingi wa kura.