Vijana wengi kati ya miaka 15-24 wanafariki nchini kutokana na UKIMWI

Vijana kati ya umri wa miaka 15 na 24 hufariki kila siku nchini kutokana na magonjwa yanayosababishwa na UKIMWI pamoja na unyanyapaa. Mwaka 2015, kulikuwa na visa 7200 vipya vya maradhi ya ukimwi huku 46% ikiwa vijana wa kati ya umri wa miaka 15 na 24. Je, pana haja ya serikali kubadilisha mbinu zake kukabili ugonjwa huu ambao unanyemelea vijana bila ya ufahamu wao? Shisia Wasilwa na kina cha taarifa hiyo.