Mgomo wa wahadhiri uliodumu kwa mwezi mzima wasitishwa

Viongozi wa muungano wa wahadhiri nchini umesitisha mgomo ambao umekua ukiendelea Kwa siku thelathini na nane sasa. Hii ni baada ya muungano huo pamoja na Baraza la vyuo vikuu vya umma kutia sahihi mkataba wa kurejea kazini.