Mwana atuhumiwa kumbaka mamake mzazi wa miaka 90 kule Makueni

Mwana atuhumiwa kumbaka mamake mzazi wa miaka 90 kule Makueni

  • Majasusi kutoka kitengo cha DCI kupitia mtandao wa mawasiliano ya Tweeter walisema kuwa mshukiwa alitoweka baada ya kudaiwa kutenda unyama huo huku mama huyo akiokolewa na kifungua mimba wake.
  • Aidha, chifu wa kata ya Nduluku, bwana Jeremiah Makau, amedhibitisha.


Polisi kule Mbooni mashariki, kaunti ya Makueni wanamzuilia mwanamume mmoja wa umri wa miaka 45 anayedaiwa  kumbaka mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 90.

Tukio hilo linatuhumiwa kufanyika usiku wa Octoba 20, wakati mshukiwa alipofika nyumbani kwa mama yake na kubisha mlango kabla ya kumtendea unyama huo pale aliporuhusiwa  kuingia  ndani ya nyumba.

 Majasusi kutoka kitengo cha DCI kupitia mtandao wa mawasiliano ya Tweeter walisema kuwa mshukiwa alitoweka baada ya kudaiwa kutenda unyama huo huku mama huyo akiokolewa na kifungua mimba wake – ambaye pia alimpelekwa katika hospitali ya Kisau anakopokea  matibabu.

 Aidha, chifu wa kata ya Nduluku, bwana Jeremiah Makau, amedhibitisha kisa hicho akisema: “Mshukiwa alikamatwa jana usiku na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mbumubuni huku uchunguzi ukiendelezwa kabla ya kufikishwa mahakamani.”