Madaktari kutoka Cuba na India kusadia Kenya

Runinga ya Citizen imeng’amua kwamba serikali za Cuba na India zinapanga kutia saini mkataba na serikali ya Kenya kuleta madaktari wataokaohudumu humu nchini hadi mgomo huo utakapoisha. Aidha mpango huu utahusisha kuletwa kwa madaktari kutoka nchi hizi mbili ili wahudumu humu nchini angalau kwa muda huku seriklai ikifanya mazungumzo na wadau kusitisha mgomo huo. Kwa upande wake, serikali ya Kenya inatarajiwa kugharamia mahitaji ya madaktari hao kakika muda watakaohudumu hapa nchini.