Dawa mpya ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI yazinduliwa

Serikali imezindua dawa itakayoweza kutumika na mtu yeyote aliyeko hatarini kuweza kuambukizika virusi vya HIV ili kujikinga na maradhi hayo pamoja na kifaa cha kupima endapo mtu ana virusi hivyo au la. Dawa hiyo inatarajiwa kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa kwa watu amabo hawana viruzi hivyo.