Isaack Hassan Asema Yuko Tayari Kung’atuka

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Ahmed Isaack Hassan amesema yuko tayari kujitoa kwenye wadhifa wake kwa muda wa siku sitini kadri ya agizo la rais Uhuru Kenyatta wiki iliyopita iwapo jina lake litakuwa kwenye orodha ya wale wanaoshukiwa kushiriki ufisadi. Hassan ameyasema haya leo baada ya kutia sahihi mkataba na shirika la dunia la kusimamia uchaguzi, jijini Nairobi. Alex Kubasu na taarifa hiyo.