Wasimamizi wapya wachukua uongozi wa hospitali ya St. Mary’s, Lang’ata

Vurugu ilizuka mapema leo katika hospitali ya St.Mary’s hapa jijini baada ya watawa wanaomiliki hospitali hiyo kuwafurusha wafanyakazi pamoja na wasimamizi wa hospitali hiyo. Na kama anavyotupasha Andrine Kilemi, mzozo huo umekua ukiendelea kwa miaka saba sasa.