Mfungwa katika gereza la Kakamega akwea paa uchi akilalamikia kupewa chakula kidogo

Mfungwa katika gereza la Kakamega akwea paa uchi akilalamikia kupewa chakula kidogo

  • Aidha Afisa huyo anahoji kuwa baadaye alishuka kwenye jengo hilo baada ya kulemewa na miale ya juu
  • Hapa gerezani wafungwa wote hupewa chakula sawa,japo wale ambao wana magonjwa na wamepewa barua na Daktari,hao tunawapa chakula kingi

Kulishuhudiwa kizaazaa katika Gereza kuu la Kakamega baada ya mfungwa mmoja anayekabiliwa na misururu ya kesi za wizi wa mabavu na mauaji eneo bunge la Matungu kujipaka kinyesi mwili wote na kisha kupanda juu ya jengo la gereza hilo akiwa uchi mnyama akilalamikia kupewa chakula kidogo.

Kisa hicho kilithibitishwa na Afisa mkuu anayesimamia Gereza Hilo Japheth Onchiri ambaye amesema kuwa mfungwa huyo alizua taharuki kwa muda akitaka kupewa chakula kingi.

Aidha Afisa huyo anahoji kuwa baadaye alishuka kwenye jengo hilo baada ya kulemewa na miale ya juu.

"Hapa gerezani wafungwa wote hupewa chakula sawa,japo wale ambao wana magonjwa na wamepewa barua na Daktari,hao tunawapa chakula kingi kutokana na idhini ya Daktari lakini bila idhini ya Daktari wanakula chakula sawa" alisema Onchiri.