Wizara ya ardhi yaeleza mikakati ya kutatua dhuluma za kihistoria

Tume ya ardhi na wizara ya ardhi zimezindua mpango wa kitaifa wa kutatua dhuluma za kihistoria zinazohusiana na umiliki wa ardhi. Mradi huo unatarajiwa kukamilika katika muda wa miaka mitano, huku walio na malalamiko wakishauriwa kuyawasilisha, huku wakielezea kwa kina walivyopoteza ardhi zao na waliofaidi. Hata hivyo mradi huo huenda ukakumbana na mawimbi ya kisiasa na kisheria, na unatarajiwa kuwagharimu walipa ushuru mabilioni ya pesa.

latest stories