Misa ya wafu ya Marehemu Askofu Cornelius Korir yaandaliwa Eldoret

Maelfu ya waumini wakatoliki walifika katika kanisa la Sacred Heart Eldoret kumpa mkono wa buriani mwendazake Askofu Cornellius Korir katika misa ya wafu. Woambolezaje walipata fursa ya kuutizama mwili wa mwendazake. Mtu waliyemwenzi, aliyekuwa Baba yao wa kiroho. Marehemu Askofu Korir atazikwa hapo kesho ndani ya kanisa hilo kulingana na tamaduni za kanisa katoliki.