MATUKIO 2017: Bwawa la Badasa

Kaunti ya Marsabit ni miongoni mwa kaunti zilizoathirika zaidi na ukame mwaka huu kiasi cha kumshawishi Rais Uhuru Kenyatta kutangaza ukame ulioathiri takribani watu milioni 2.7 kuwa janga la kitaifa. Licha ya dharura hiyo iliyohitaji mataifa ya kigeni kutoa misaada ya chakula, ahadi ya serikali ya kununua mifugo wa wenyeji wa kaunti hiyo ili kuwaepushia hasara, ilisalia kuwa ahadi tu. Na kama anavyoarifu Kadzo Gunga bwawa la Badasa lililokuwa tegemeo la wenyeji halijakamilika miaka kumi baada ya karandasi kutolewa.