Benki Kuu yaagiza kutekeleza sheria mpya kuanzia Sep 14

Benki za biashara humu nchini zimepewa makataa ya wiki mbili kupunguza viwango vya riba kwa mikopo. Benki kuu ilitoa ilani hiyo kupitia barua kwa wamiliki wa benki na taasisi zingine za kifedha na kuonya kuwa watakaokiuka sheria hii watatozwa faini ya shilingi milioni moja au kifungo cha mwaka mmoja. Mwanahabari wetu wa maswala ya biashara Denis Otieno atufungulia jamvi letu la nipashe.