Uhuruto wakabiliwa na kibarua kigumu kuteua wandani wao

Huku macho ya taifa nzima yakielezewa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, wanapojiandaa kuiweka wazi orodha ya wanaopendekezwa kujumishwa kwenye baraza la mawaziri, kampeini kali za kusaka bendera zinaendelea nyuma ya pazia. Duru zimearifu kuwa angalau mawaziri 10 kati ya 19 wanaohudumu kwa sasa watapigwa kalamu, huku kibarua kwa Kenyatta na Ruto kikiwa kuamua utendakazi bora, usawa wa kimaeneo na kijamii na kuwazawadi walioshiriki pakubwa kuwatafutia kura.