Chama kipya cha Jubilee chazaliwa

Hatimaye chama kipya cha Jubilee kimezinduliwa rasmi hii leo na Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake Wiliam Ruto katika hafla za aina yake huko Kasarani. Ingawa wengi walikusanyika kwa ajili ya kumkaribisha mwana mpya wa kisiasa ni wazi kuwa safari ya chama hicho kipya inatarajiwa kuwa na changamoto nyingi na kama anavyotupasha Salim Swaleh, zoezi la kura ya mchujo ni moja ya mambo yanayowakuna vichwa viongozi wakuu wa Jubilee