MATUKIO 2017: Waandishi wa habari wa RMS wasimulia ajali ya ndege

Tarehe 17 mwezi Julai mwaka huu, waandishi wa habari wa runinga ya Citizen; Sam Ogina na Mauritius Oduor pamoja na Joseph Njane wa Radio Citizen waliabiri ndege kutoka uwanja wa Wilson hapa jini Nairobi kulelekea Baringo ili kuandaa taarifa za kisiasa za muungano wa NASA. Hata hivyo, safari hiyo ilikatizwa ghafla baada ya ndege waliyoabiri kuanguka. Wanahabari hao pamoja na marubani walijeruhiwa, na baadaye wakatibiwa. Ingawa hatukuwapata marubani, waandishi hao wa habari leo wanasimulia kisa hicho katika makala ya matukio ya mwaka wa 2017.