NASA kurejelea maandamano wiki ijayo

Muungano wa NASA sasa umeashiria kuwa wafuasi wake watarejelea maandamano wiki ijayo. Mikutano ya viongozi wa NASA leo, imepanga mikakati ya maandamano hayo ambayo yanadhamiria kuonyesha kutoitambua serikali. Kadhalika NASA inapanga orodha ya bidhaa na huduma zitakazosusiwa na wafuasi wake ikiwa ni pamoja na majengo ya kibiashara ambayo imetundika picha ya Rais Kenyatta. Viongozi wa Jubilee wanamtaka kinara wa nasa Raila Odinga kulegeza msimamo kulisaidia taifa kusonga mbele.

latest stories