Watu 38 wafariki kwenye ajali iliyotokea alfajiri eneo la Migaa

Wizara za uchukuzi na usalama wa taifa zimesitisha safari za usiku za magari ya uchukuzi wa umma kufuatia ajali iliyowaua wakenya 38 huko Migaa katika barabara ya Nakuru kwenda Eldoret. Waziri wa uchukuzi James Macharia anasema hatua hiyo itadhibiti ongezeko la maafa barabarani. Haya yanajiri huku maswali yakiibuka kuhusu kampuni ya Nairobi Bus iliyohusika katika ajali hiyo, baadhi ya manusura wakiarifu walikuwa wametoa onyo kwa dereva apunguze kasi lakini hawakusikilizwa.

latest stories