Watu 9 kutoka familia moja wafariki katika ajali ya barabarani

Hata baada ya mikakati kuwekwa kudhibiti ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku usafiri wa umma wakati wa usiku, Watu tisa wamepoteza maisha yao katika ajali nyingine ya barabarani usiku wa kuamkia leo. Inasemekana kwamba waathiriwa hao ambao ni wa familia moja walifariki baada ya matatu waliokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo eneo la Ndaragwa katika bara bara ya Nyeri kuelekea Nyahururu.