Mgombea wa urais Abduba Dida apata pigo

Tuangazie nyanja za kisiasa ambapo ni rasmi kuwa mdahalo wa urais mwaka 2017 utaendelea kuandaliwa. Hii ni baada ya mahakama kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa kortini na mwaniaji urais Abduba Dida kupinga mpangilio wa mdahalo huo.
Kufuatia hatua hii kamati andalizi ya mdahalo huo imeahirisha mdahalo wa kwanza kutoka tarehe 10 mwezi huu hadi tarehe 24 mwezi huu wa saba. Haya yanajiri huku raila odinga akidhibitisha kushiriki mdahalo huo. Patrick Igunza anayo taarifa hiyo.