Uhuru aandaa kikao na rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi

Mataifa ya Kenya na Misri hii leo yamekubaliana kuimarisha uhusiano baina yao katika nyanja mbalimbali hususan maswala ya uchumi na biashara.
Wakiwahotubia wanahabari katika Ikulu ya Nairobi Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Misri Abdel Fattah El-Sisi wameahidi kukamilisha makubaliano yatakayorahisisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa kutoa vikwazo.

latest stories