Mhudumu wa bodaboda azuiliwa kwa tuhuma za kumuua msichana wa kidato cha nne

Mhudumu wa bodaboda azuiliwa kwa tuhuma za kumuua msichana wa kidato cha nne

  • Alitupigia simu saa moja usiku akisema amefika Shianda akaabiri pikipiki na atafika nyumbani muda mfupi ujao.
  • Juhudi zao kumtafuta zimekuwa zikiambulia patupu ila walivutia na posti moja kwenye mtandao wa kimarafiki wa Facebook ambako mshukiwa alikuwa ameposti picha yake kwenye accounti ya mwendazake.
  • Siku chache baada ya mwathiriwa kupotea tulishangaa kuona mshukiwa kaposti picha yake kwenye accounti ya mwendazake

Mwanaume mmoja, mkaazi wa kijiji cha Emanyasa eneo bunge la Mumias mashariki, anazuiliwa na maafisa wa polisi wa kituo cha Mumias kwa tuhuma za mauaji.

John Odinga, 27 ambaye ni mhudumu wa bodaboda katika kituo cha Shianda anaripotiwa kumuuwa Cyncia Makokha 17, mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya upili ya Kibera mjini Nairobi.

Kulingana na Chrispinus Makanga na Florence Wanga (wazazi) wanasema mwendazake alikuwa kasafiri kutoka mjini Nairobi, anakosoma, kuhudhuria hafla ya matanga ya nyanyake Jumatatu tarehe 4 alikoabiri pikipiki ya mshukiwa akitaka amfikishe nyumbani kwao kabla ya wawili hao kutoweka.

“Alitupigia simu saa moja usiku akisema amefika Shianda akaabiri pikipiki na atafika nyumbani muda mfupi ujao,"akasema Makanga.

Kwa kawaida safari kutoka Shianda hadi kwao nyumbani ingewagarimu takriban dakika 20 ila walishangaa lisani moja lilikuwa limepita na hakuwa amefika wala simu yake haikuwa inaingia.

Juhudi zao kumtafuta zimekuwa zikiambulia patupu ila walivutia na posti moja kwenye mtandao wa kimarafiki wa Facebook ambako mshukiwa alikuwa ameposti picha yake kwenye accounti ya mwendazake.

“Siku chache baada ya mwathiriwa kupotea tulishangaa kuona mshukiwa kaposti picha yake kwenye accounti ya mwendazake. Tulianzisha uchunguzi tukampata mshukiwa na simu ya mwendazake,” akasema Wanga.

Kwa msaada wa maafisa wa polisi walifanikiwa kuvamia makaazi ya mshukiwa walikomkamata na vitu vingine vya mwathiriwa vikiwemo nguo pamoja na vyakula alivyonunuwa kutumika kwenye hafla ya matanga ya nyanyake.

Michael Omwanda ni mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda shianda na anasema kando na mshukiwa kuhusishwa kwa visa vya wizi wa watoto eneo hilo pia amekuwa akiwahangaisha wakaazi kwa kuwaibia vitu vyao ila kila wakimripoti amekuwa akiwachiliwa kwa misingi zisizoeleweka.

“Aliwai shtakiwa na kuachiliwa kwa kosa la kuwaiba na kuwasafirisha watoto wawili hadi mjini Busia kwa lengo la kuwauza,”akasema.

Akidhibitisha kukamatwa kwa mshukiwa, kaimu chifu wa Bumini Winstone Shirebo amewataka wenyeji kuwa watulivu uchunguzi ukianzishwa huku mshukiwa akisubiri kufikishwa mahakamani.

Mwili wa mwendazake ulipatikana siku nne baadaye ukielea juu ya maji ya mto Lusumu na wapita njia waliopiga ripoti kwa maafisa wa polisi wa kituo cha Mumias waliouzoa na kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya rufaa ya kakamega ukisubiri kufanyiwa upasuaji

latest stories