Wenyeji wa kaunti ya Lamu wanaoishi msitu wa Boni walazimika kuhama makwao

Wenyeji wa kaunti ya lamu hususan kutoka  msitu wa boni, wamelazimika kuyahama makao yao na kuishi katika kambi za wakimbizi katika eneo la witu.

Hii ni kufuatia amri ya kamishna wa kaunti hiyo ya lamu, Joseph Kanyiri, ambaye amesema lengo ni kutekeleza operesheni ya kupambana na wanamgambo wa kundi la kigaidi la alshabaab.