Wazee Wa Waluo Wamrai Awanie Useneta Homa Bay

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ametoa dalili tosha kuwa yuko tayari kuwania kiti cha useneta cha kaunti ya Homabay. Raila ambaye hii Jumapili ametembelewa bomani kwake kijiji cha Opoda, Bondo kaunti ya Siaya na baraza la wazee wa jamii ya Waluo kutoka kaunti ya Homabay. Wakati wa mazishi wa marehemu Otieno Kajwang’ ambaye anapania kumrithi alisema kuwa sio lazima atakayemrithi awe anatoka kwenye familia ya marehemu seneta Kajwang’. Ingawa hakutangaza msimamo wake, mkurugenzi wa uchaguzi katika chama cha ODM Junet Mohammed na mwenyekiti wa chama hicho John Mbadi wamedokeza kuhusu uwezekano wa Raila kuwania kiti hicho ili kukiongeza chama cha ODM umaarufu katika seneti  na uongozi wa taifa.