Wasichana zaidi ya 60 walibaki shuleni kwa hofu ya kukeketwa

Minyororo ya itikadi za utamaduni imemfunga msichana katika jamii mbalimbali nchini ikiwemo ya wamaasai kwa muda mrefu. Lakini sasa vita dhidi ya uovu huo vimemepigwa jeki na vituo vya shule za kuwanusuru wasichana kutoka mila potovu ya ukeketeji na ndoa za mapema katika eneo la Kajiado ya kati.