Washukiwa 17 wa kashfa ya NYS wafikishwa mahakamani

Aliyekuwa katibu mkuu katika wizara ya ugatuzi Peter Mangiti amewachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu huku maafisa wa usalama wakianzisha shughuli ya kuwasaka maafisa wawili wakuu wa zamani wanaohusishwa na sakata ya NYS. Aden harakhe ambaye alikuwa naibu mkurugenzi mkuu wa NYS na Hassan Noor aliyesimamia kamati ya zabuni katika wizara ya ugatuzi anasakwa baada ya kususia kikao cha kufunguliwa mashtaka pamoja na wengine 22 kuhusiana na zabuni iliyotolewa kinyumbe na sheria kwa gharama ya shilingi milioni 47.6