Wakurugenzi wa Benki ya Chase waliiba sh bilioni 33

Inakisiwa kuwa shilingi bilioni 33 ziliporwa katika benki ya chase na sasa benki kuu iko kwenye harakati za kusaka pesa hizo kutoka kwa wakurugenzi wakuu na wanahisa wanaohusishwa. Stakabadhi ambazo  nipashe imezipata zinaonyesha kuwa waliokuwa wakurugenzi na wana hisa  walishirikiana kuilaghai benki hiyo pesa hizo katika sakata inayowahusisha watu wengine sita na kampuni 11.