Wagonjwa zaidi walalamikia mateso hospitalini Kenyatta

Ziara ya wabunge wanawake katika hospitali ya kitaifa Kenyatta yafichua mateso zaidi wanayopitia wagonjwa ikiwa ni pamoja na kulala sakafuni na dhulma zinginezo. Kwa wagonjwa wanaolazwa bado kizungumkuti kinaendelea kushuhudiwa katika hospitali kuu ya Kenyatta kufuatia mjadala uliozuka hapo jana katika mitandao ya kijamii kuhusu wanawake waliojifungua kubakwa na wahudumu wa vyumba vya kuhifadhi maiti.