Wabunge watakiwa kuidhinisha ripoti bila mabadiliko

Bunge la kitaifa limeidhinisha ripoti ya kamati teule kuhusu mabadiliko ya sheria za uchaguzi, licha ya kuondoa kipengee kilicholenga kuharamisha mtindo wa wanasiasa kuhamahama vyama. Ilibidi naibu wa spika Dkt. Joyce Laboso kuwanyima wabunge nafasi ya kuifanyia ripoti hiyo mabadiliko zaidi, ili kuhifadhi maafikiano kati ya Jubilee na Cord katika kamati teule. Sasa bunge litaanza kujadili miswada miwili, inayolenga kulainisha maandalizi ya uchaguzi wa mwaka ujao, haswa uteuzi wa makamishna wapya wa tume ya Iebc.